Taarifa na Salim Mwakazi
Kwale, Kenya, Juni 26 – Mwakilishi wa Kike kaunti ya Kwale Zuleikha Hassan amewataka viongozi wa kisiasa kuangazia zaidi maswala ya maendeleo kwa wananchi badala ya kupiga siasa zisizokuwa na msingi wowote.
Zulekha amesema wakenya wanapitia shida nyingi mashinani kutokana na kutoangaziwa kwa kina maswala ya maendeleo, akiwataka viongozi hao kusitisha siasa na kuinua uchumi wa wananchi.
Akizungumza kule Diani kaunti ya Kwale, Bi Zulekha amesema iwapo viongozi wa kisiasa watambua magangaiko wanaopitia wananchi basi taifa hili litapiga hatua kimaendeleo.
Wakati uo huo ameunga mkono pendekezo la Waziri wa Fedha nchini Henry Rotich la kuwataka wahudumu wa bodaboda kuwa na bina, akisema hatua hiyo ni mwafaka japo akazitaka kampuni za bima kuhakikisha zinazingatia sheria ya fidia.