Picha kwa hisani –
Mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kwale Bi Zuleikha Hassan amemkosoa Naibu Rais Dkt William Ruto, akisema hawezi kuliongoza taifa hili.
Akizungumza na wanahabari Zuleikha amesema Ruto amekosa agenda za kuimarisha maisha ya taifa hili akiwataka Wakaazi wa Kaunti ya Kwale kutomuunga mkono kiongozi huyo.
Kulingana na Mwakilishi huyo wa kike, taifa hili linahitaji mwelekeo wa kiuchumi, kiuongozi na kidemokrasia ambao Ruto hawezi kuwapa Wakenya.