Picha kwa hisani –
Mwakilishi wa wanawake kaunti ya Kwale Zulekha Hassan amewataka wakaazi wa Kwale kujitokeza na kuunga mkono ripoti ya BBI iliowasilisha rasmi kwa Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga.
Zulekha amesema ripoti ya BBI imepatia nguvu zaidi bunge la Seneti na ile la kitaifa katika kufanikisha maswala muhimu nchini yanayomuhusu Mwananchi mashinani.
Kiongozi huyo amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo na Pwani kwa jumla kuhakikisha wanaisoma ripoti hiyo kwa kina zaidi kabla ya kufanya maambuzi hayo.
Wakati uo huo, Kiongozi huyo amesema swala la BBI litachangia zaidi kukabiliana na swala la ufisadi na kuchangia usambazaji wa fedha hadi mashinani kwa ajili ya kufanikisha maendeleo.