Picha kwa hisani
Mwanamuziki wa Bongo Flava kutoka recording label ya Wasafi Classic Beiby maarufu kama WCB, Zuchu amezungumzia ukaribu wake na Rich Mavoko, msanii ambaye alitoka WCB miaka miwili iliyopita baada ya kutoelewana kikazi na management hiyo. Zuchu alisajiliwa na recording label hiyo mwezi April mwaka huu baada ya Mwanamuziki Harmonize kutoka WCB.
Akizungumza kwa kipindi cha Kaya Flavaz, kupitia njia ya simu, Zuchu amefichua kwamba mbali na wasanii wa WCB, ingekuwa rahisi kwake kufanya collabo na Rich Mavoko kwani alikuwa rafiki yake sana kipindi kile alipokuwa WCB, na kuwa mwenye kumtia moyo na ni kati ya wanamuziki waliokuza talanta yake.
“Kati ya Harmonize, Rich Mavoko na Q boy msafi, Namchagua Mavoko kwa sababu ni mmoja kati ya wasanii ambao walinitia moyo na kuikuza talanta yangu, kipindi kile yuko WCB. Yaani yeye alikuwa my number one fan…”
Mwanamuziki huyo pia alieleza kuwa amefanya kazi na Wasafi kwa miaka minne sasa na alipewa nafasi za kujiunga na recording zingine lakini alichagua Wasafi kwani anahisi ndio bora zaidi na anapenda utaratibu wao ya kufanya kazi.
Aidha, Zuchu pia aliweka wazi kukerwa na dhana na gumzo linaloendelea la kuwa katika uhusiano na msanii yoyote kutoka WCB akiitaja kama tabia mbaya ya kushusha hadhi wa wanamuziki.