Story by Janet Shume –
Shirika la uhifadhi wa misitu nchini linaendeleza upanzi wa miti katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Kwale kuhakikisha inafikia ajenda kuu ya serikali ya asilimia 10 ya misitu nchini.
Afisa katika Shirika hilo kaunti ya Kwale Edwin Misache amesema zoezi hilo ambalo linaendelea katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Kwale ikiwemo Kinango ni kupitia ushirikiano na idara mbalimbali na mashirika ya kijamii.
Masiche amesema Shirika la misitu kaunti ya Kwale inalenga kupanda miti zaidi hata maeneo ya kandokando ya barabara ili kuongeza idadi ya misitu nchini.
Hata hivyo amesema licha ya visa vya uharibifu wa misitu nchini kushuhudiwa kupungua, Shirika hilo linaendeleza ushirikiano wa hali ya juu na maafisa wa Shirika la uhifadhi wa wanyamapori nchini KWS.