Story by Our Correspondents
Idadi ya wakaazi wanaojitokeza kwa uchaguzi wa ugavana katika kaunti ya Mombasa kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura imeonekana kuwa chini mno.
Licha ya baadhi ya vituo vya kupigia kura katika kaunti hiyo vimefunguliwa tangu mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi ili kufanikisha uchaguzi huo wa ugavana bado idadi ya watu wanaojitokeza kwa uchaguzi huo iko chini.
Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kupitia maafisa wake imesema imejipanga vyema kuhakikisha uchaguzi huo wa ugavana katika kaunti ya Mombasa unaandaliwa vyema bila ya pingamizi zozote.
Aidha wamewataka wakaazi wa kaunti hiyo kutopuuza zoezi hilo na badala yake kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanatekeleza jukumu lao la kikatiba la kushiriki zoezi hilo la uchaguzi wa ugavana wa Mombasa