Zoezi la kusajili makurutu wa shirika la huduma kwa wanyamapori nchini KWS linaendelea kwa sasa katika kaunti mbali mbali za pwani na kwengineko nchini.
Afisa mkuu wa KWS anaesimamia zoezi hilo kaunti ya Kwale Jacob Olerali amesema wanatarajia kusajili vijana 76 kati ya vijana zaidi ya 3,900 walijitokeza kushiriki zoezi hilo ,akisema wataendeza zoezi hilo kwa uwazi.
Jacob amesema makurutu watakaosajiliwa na shirika hilo hii leo watasaidia kulinda hifadhi za wanyamapori na misitu ya kaunti zote 47 nchini,akisema serikali imetenga fedha kusimamia mpango huo.
Kwa upande wao vijana waliojitokezza kushiriki zoezi hilo wakiongozwa na Lilian Mwadingo wamekosoa zoezi hilo, wakisema KWS ingewachuja waliotuma maombi ya kazi hio ili kupunguza idadi ya wanaokashiriki zoezi hilo