Story by Our Correspondents-
Agizo lililotolewa na Mahakama ya upeo la kuhesabiwa upya na kuchunguzwa kwa kura zilizopingwa katika vituo 15 vya kupigia kura ikiwemo eneo bunge la Mvita kaunti ya Mombasa, masanduku ya kura hizo za urais zimewasilishwa katika Mahakama ya Milimani.
Tume ya IEBC kupitia Mawakili wake wakiongozwa na Wakili Githu Muigai wamewasilisha masanduku hayo huku zoezi hilo likisimamiwa na msajili wa mahakama hiyo kwa usaidizi wa maafisa wa usalama.
Agizo hilo lililotolewa na Jaji Isaac Lenaola, ni kuweka wazi tashishwi zilizowasilishwa na mlalamishi wa kesi hiyo Raila Odinga dhidi ya tume ya IEBC na Mwenyekati wake Wafula Chebukati.
Maafisa wa idara ya Mahakama sawa na wale wa masuala ya teknolojia wanaendeleza zoezi hilo la mda wa saa 48 na kuwasilisha ripoti ya ukaguzi na hesabu ya kura hizo kama zinaambatana na zile zilizopakuliwa katika tovuti ya IEBC hasa fomu 34A.
Majaji hao wa Mahakama ya upeo wanatarajiwa kutoa uamuzi wao kuhusiana na kura hizo kama tume ya IEBC ilizingatia usawa katika utendakazi wake hasa swala la uwazi, haki na usawa wakati wa upigaji kura.