Bifu kati ya wanamuziki kutoka kaunti ya Mombasa Ziky Mtanah na imepamba moto mitandaoni baada ya wawili hao kujibizana vibaya na Emlend kufichua siri za Ziky. Ziky amejipata pabaya baada ya kumwandikia mwanamuziki wa kike Keyla Kendi ujumbe wa mapenzi kupitia ukurasa wake wa FaceBook akimtaka kumkubalia na kuingia kwenye mahusiano naye.
“Kama kuna mwanamke naeza pigania kumpata na hata kumuoa awe mke wangu ni Keyla Kendy… Please mpeni ujumbe wangu kua nko kwenye kampeni ya kumtafuta na nko tayari kwa chochote kitakacho nikumba ili kumpata .. nimejikaza ila sasa muda umefika kupigania kile moyo wangu unapenda .” – Ziky
Kauli hiyo ya Ziky ilimuudhi Emlend ambaye mbali na kuwa mwanamuziki anayerecord studio moja na Keyla, ni manager wake na sasa hivi anadai kuwa mpenzi wa msanii huyo. Jambo lililompelekea Emlend kumjibu Ziky na kufichua jinsi alivyofukuzwa kwa Akothee kwa tabia yake ya uzembe.
“Naskia kuna mc flani ametutusi.. eti tulipoteza Keyla Kendy kwenye mziki.. na heri sisi ye kafukuzwa kama Kuku kwa Akothe… kwa kukimbiza madem vikojozi kama Kimbuzi.. Ziky Mtanah usifanye nianze kukuanika hapa vi inbox vyako tokea ukiwa tandiko wa tandiko. Hivi ni nani alikubadilisha hilo jina kama sio Emmydee na mimi.. sai umekuwa star sio…” – Emlend
Hata hivyo, Ziky alijitetea kuwa anampenda Keyla kwa dhati na anamatamanio ya kumuoa. Aliendelea kwa kumsuta Emlend akimuonya akae kando kwani yeye ni manager wa Keyla tu na wala siyo mume wake.
Makubwa…