Wanamuziki kutoka Tanzania wameonekana kupenda beat ya ngoma ya Zee aliyomshirikisha Hamadai wa the Mafix kwa jina ‘Nakuja’ iliyoachiwa tarehe 13 July, 2019, na kuandika nyimbo zenye melody kama yake. Mashabiki wa muziki wa bongo flava, Afrika Mashariki walionyesha upendo wao kwa kuufanyia “challenge” kwenye mtandao wa Instagram.
Hata hivyo, kwa sasa ngoma hio imetazamwa na watu zaidi ya milioni 2.5 katika mtandao wa YouTube. Hii ni moja kati ya ngoma ambazo inaonekana wazi kwamba wasanii walitamani sana melody yake.
Miezi tisa baadae, msanii Chipkizi anayefanya vyema ndani na nje ya Tanzania Marioo alizidiwa na mapenzi ya wimbo huo, na hivyo akaamua kufanya ngoma yake kwa jina “Unanikosha” kwa kutumia melodi ya ‘Nakuja’. Unanikosha ni ngoma ambayo kufikia sasa imetazamwa na watu zaidi ya laki saba katika mtandao wa youtube.
Haikuishia hapo, mwanamuziki aliyekuwa katika recording lebo ya wasafi (WCB) na anaemiliki lebo ya ‘Konde Gang’ maarufu Harmonize pia ameonyesha kupagawishwa na melodi ya ‘Unanikosha’ na kuachia kazi yake mpya “falling in love” ambayo iliwekwa kwa mtandao wa YouTube tarehe 26 Mei, mwaka huu, video vixen akiwa ni mpenzi wake Sarah.
Hata hivyo, kwa ukubwa wa jina lake tayari wimbo huo umetazamwa na zaidi ya watu milioni 1.2 katika mtandao wa YouTube ndani ya wiki moja. Tangia aachane na lebo ya wasafi, msanii huyu kutoka Bongo amekuwa akihusishwa na kashfa ya wizi wa nyimbo ikiwemo ngoma ya my bedroom ambayo wanamuziki wakongwe kutoka Pwani ya Kenya walilalama kuibiwa.
Je, una maoni gani kuhusu msanii kufanya wimbo kutumia beat ama melody ya msanii mwingine?