Story by Hussein Mdune-
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini limesema takribani wakaazi laki mbili wanakabiliwa na baa la njaa katika kaunti ya Kwale.
Kulingana na Afisa wa Shirika hilo tawi la kaunti ya Kwale Mohammed Mwainzi, idadi kubwa ya walioathirika zaidi ni akina mama wajawazito, watoto na wazee.
Mohammed amesema kama shirika tayari wanashirikiana na wahisani mbalimbali ili kuhakikisha wakaazi wanapata chakula na maji.