Story by Salim Mwakazi –
Jumla ya watu 49 wamekamatwa na kushtakiwa Mahakamani katika oparesheni ya kukabiliana na biashara ya pombe haramu kaunti ya Kwale.
Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Ambrose Steve Oloo amesema maafisa wa polisi wamefanikiwa kumwaga zaidi ya lita 1,500 ya pombe katika oparesheni hiyo iliozinduliwa na serikali.
Wakati uo huo, amehoji kwamba zaidi ya misokoto 165 ya bangi pia imenaswa katika oparesheni hiyo.
Afisa huyo wa polisi amebainisha kuwa tayari watu watatu waliopatikana na bangi hiyo wamefikishwa mahakamani.