Story by Mwanaamina Faki-
Shirika la msalaba mwekundu limesema takriban wakaazi elfu 20 kutoka maeneo bunge ya Kinango na Lungalunga kaunti ya Kwale walioathirika na kiangazi, wamepata msaada wa kifedha na chakula kutoka kwa shirika hilo.
Akizungumza na Wanahabari Mshirikishi wa shirika hilo kaunti ya Kwale Mohamed Mwaenzi amesema mradi huo wa kuwakimu waathiriwa wa baa la njaa ulianza mwaka uliopita na unatarajiwa kukamilika rasmi mwezi huu.
Mwaenzi amesema katika mradi huo shirika hilo limenunua mifugo kadhaa kutoka kwa wafugaji wa maeneo hayo kame ili kuwaepushia hasara kutokana na kufariki kwa mifugo kufuatia makali ya kiangazi.