Picha kwa hisani –
Wahudumu wa afya zaidi ya 30 wameripotiwa kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona katika kaunti ya Taita Taveta.
Wahudumu hao wa afya wanasema upungufu wa wafanyikazi katika kaunti hiyo, ndio kumechangia pakubwa maambukizi hayo.
Hapo awali muungano wa wahudumu wa afya nchini KMPDU, ulishikilia msimamo wake wa kushiriki mgomo ifikapo Jumatatu juma lijalo, iwapo matakwa yao hayataangaliwa.
Wahudumu hao wa afya wanalalamikia ukosefu wa vyombo bora vya kuwakinga na maambukizi hayo.