Picha kwa hisani –
Naibu wa Rais William Ruto hii leo anatarajiwa kukutana na viongozi zaidi ya mia moja ikiwemo wabunge na maseneta nyumbani kwake Karen,Nairobi kujadili masuala mbali mbali ikiwemo azma yake ya kuwania urais kwenye uchaguzi ujao.
Kulingana na mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro kwenye kikao hicho pia watajadili jinsi ya kuimarisha makali yao katika mabunge yote mawili wakati huu ambapo vikao vya bunge vinatarajiwa kurejelewa hapo kesho.
Akizungumza hapo jana Osoro vile vile amesema watazungumzia kuhusu ripoti ya kufanyia mabadiliko katiba ya nchi ya BBI,miongoni mwa masuala mengine yakuimarisha upande wa Naibu wa Rais kisiasa.
Naye mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amesema viongozi wa Jubilee wanaoegemea upande wa naibu wa rais William Ruto wanakandamizwa na kwamba kwenye kikao hicho watakubaliana iwapo watasitisha kutoa mchango wa kila mwezi katika chama hicho.