Story by Ali Chete –
Zaidi ya vijana 600 katika eneo la Nyali kaunti ya Mombasa wamenasuliwa kutoka kwa makundi ya kihalifu.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kuwapokea vijana hao, Naibu Kamishna wa gatuzi dogo la Nyali Henry Rop amesema kupitia miradi mbalimbali kutoka kwa mashirika ya kijamii pamoja na chuo kikuu cha Kenya Methodist vijana wengi wamekubali kuasi uhalifu.
Rop amesema juhudi hizo zitaendelezwa ili kuhakikisha vijana waliojiunga na makundi ya kihalifu wanajisajilimisha na kusaidia kujikimu kimaisha kwani njia ya kuwaweza kujinasua ni kuwaongelesha na wala sio kutumia nguvu.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa chuo cha Kenya Methodist Winfred Githinji amesema wameamua kushirikaina na jamii ili kuwanasua vijana kutoka kwa uhalifu na kuwapa mafunzo na kubuni ajira.