Zaidi ya vijana 350 Wanachama wa makundi mbalimbali ya kihalifu katika Kaunti ya Mombasa wamefikishwa mahakamani katika kipindi cha mwezi mmoja uliyopita.
Mshirikishi mkuu wa utawala katika Kaunti ya Mombasa John Elungata amesema hatua hiyo inafuatia oparesheni kali ya kiusalama iliyoimarishwa katika pembe zote za Kaunti hiyo.
Kulingana na Elungata, oparesheni hiyo imeimarishwa huku kikosi maalum cha Maafisa wa usalama kikipiga kambi katika maeneo yanayoshuhudia msururu wa visa vya uhalifu yakiwemo yale ya Likoni na Kisauni.
Elungata hata hivyo amewahakikishia wageni wanaotembelea eneo la Pwani ili kujivinjari msimu huu wa likizo ya mwisho wa mwaka kamwe kutokuwa na hofu yoyote kwani swala la usalama limezingatiwa.