Picha kwa hisani –
Wizara ya elimu nchini imeweka wazi kwamba kufikia sasa wanfunzi 17 na waalimu 33 wameambukizwa virusi vya corona tangu shule kufunguliwa kwa wanafunzi wa gedi ya nne,darasa la nane na kidato cha nne.
Akizungumza mbele ya kamati ya bunge la kitaifa kuhusu elimu hapo jana,Katibu katika wizara hiyo Belio Kipsang amesema zaidi ya shule 35 kote nchini zimeripoti visa vya maambukizi ya virusi vya Corona.
Kipsang amesema serikali haina mipango yoyote ya kuzifunga shule licha ya idadi ya visa vya maambukizi kuongezeka na kwamba wanaendelea kuidhinisha mikakati ya kudhibiti maambukizi katika shule za humu nchini..
Kipsang amehakikishia wadau wa elimu kwamba mikakati mwafaka inaendelezwa na Wizara ya Elimu kuhakikisha usalama wa wanafunzi unaangaziwa.