Picha kwa hisani –
Kamati inayosimamia zoezi la kukusanya sahihi ili kuidhinisha mchakato wa BBI na kufanikisha kuifanyoa marekebisho Katiba, sasa inadai kuwa imekusanya zaidi ya saini milioni 1.5 kufikia sasa.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Junet Mohamed na msaidizi wake Denis Waweru amesema zoezi hilo linaendelea vyema kote nchini tangu lilipozinduliwa na Rais Uhuru Kenyatta na Kinara wa ODM Raila Odinga.
Junet amesema kufikia mwisho wa wiki hii, Kamati hiyo itakuwa imekusdanya saini milioni nne huku akiwahimiza wakenya kutopuuza zoezi hilo na badala yake wajitokeza ni kulifanikisha.
Katika kaunti ya Kilifi, Gavana wa kaunti hiyo Amason Jeffa Kingi ameongoza zoezi hilo huku akisema watu zaidi ya elfu 35 katika kaunti hiyo wametia saini nakala za zoezi hili na akawataka wakaazi kujitokeza na kutia saini kwa hiari.
KINGI – SAHIHI 30 11 20
Kwa upande wake, Kamishna wa kaunti hiyo Kutswa Olaka amesema zoezi hilo linaendelea vyema huku akiwataka wakaazi kuhakikisha wanazingatia swala zima la usalama.