Familia elfu nane katika kaunti ya Kwale, zilizosambaratika kiuchumi kutokana na janga la Corona zitanufaika na chakula cha msaada katika awamu ya kwanza ya mradi huo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema wanatarajia kupata msaada zaidi kutoka kwa wahisani na wakaazi zaidi watapata msaada huo.
Amesema msada huo utatolewa kwa wananchi kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na serikali na kwamba suala la kudumisha umbali wa mita moja na zaidi utazingatiwa wakati wa zoezi hilo.
Kauli yake inajiri huku baadhi ya wakaazi wa kaunti hio wakilalamikia kubaguliwa katika mpango huo licha ya kuwa na uhitaji wa msaada.