Msanii aliyesifika na kibao Binti Kiziwi Z Anto amefunguka na kuweka wazi kuwa kwa kiasi fulani mziki ulimshinda.
Akizungumza jijini Dar es Salaam akiwa katika harakati za kurejea tena kwenye ulingo wa tasnia ya burudani, Z Anto amesema kuwa gharama za mziki zilikuwa kubwa kwake hali iliyomfanya kukimbilia uwekezaji mbadala kando na mziki.
Msanii huyo amefichua kuwa alifungua sehemu za kukodi ambazo mpaka sasa zinaendelea kumpa kipato.
Aidha amesema kuwa tofauti yake na wasanii wakubwa kama Ali Kiba na Diamond ni ndogo sana na anahisi yupo n auwezo wa kurudi na kuchukua tena soko la mziki wa Bongo Fleva.
Je unadhani bado yupo na nafasi?