Picha Kwa Hisani –
Duuhh!! Mlole classic kaja na jipya. HIvi, kwani kuna bifu kati ya mlole classic na yuro Millionaire? Gumzo limetanda mitandaoni baada ya picha za mahaba za mwanamitindo anaefahamika kwa jina Esther Kioko ambaye inadaiwa kuwa mpenzi wa Yuro millionare kuendelea kusambaa. Kinacho umiza mioyo ya mashabiki wengi ni jinsi Mlole anavyoonekana katika picha hizo akishikashika na kumtomasa mrembo huyo licha ya yeye kufahamu uhusiano uliopo baina ya mwanamitindo huyo na star wa maflava a.k.a Yuro millionaire.
Si mara ya kwanza kwa mwana mitindo huyo kukumbwa na scandal, iliwahi kutokea wakati wa uzinduzi wa video ya Yuro “basi iwe” lakini wakati huo wazazi wake ndio walikuwa na shida.
Wanasema hakuna mwamume shujaaa mbele ya mwanamke mrembo, ni wazi lakini ni nini hasa kilichompelekea mlole kufanya hivyo? Kwanza nyimbo iliyofanyiwa video sio mpya, ni wimbo wa zamani. Je, mazoea na urafiki wa Mlole na Esther yalianza lini?
“Zuzu” ndio shida, na zuzu ndio jina la wimbo huo ambao ulifanyiwa video. Na sasa mashabiki wamegeuza jina hilo la zuzu na kumbandika yuro huku wengi wakidai kwamba hana usemi wowote katika mahusiano hayo na hivyo amefanywa zezeta. Hata hivyo kwa upande wa mashabiki wa Yuro, wengi wameonekana kumtetea wakisema ni vyema alivyo fanya hasa kumpa nafasi mpenzi wake kuendeleza taaluma yake huku wakisistiza kwamba ni video tu wala hakuna lolote.
Kwa upande wake Yuro bado hajazungumza chochote, lakini wewe unahisi vipi na alichokifanya Mlole Classic? Kwa mengi zaidi kuhusiana na kasumba hii, unaeza kuitazama video ya wimbo huo kupitia youtube channel ya Mlole Classic na uache comment yako.