Story by Gabriel Mwaganjoni-
Vyama tanzu ndani ya Muungano wa Azimio la Umoja One Kenya katika kaunti ya Mombasa vimehimizwa kushirikiana ili kuhakikisha mgombea wa urais wa Muungano huo Raila Odinga anashinda uchaguzi mkuu.
Mgombea wa ubunge wa Nyali kwa tiketi ya Chama cha Jubilee Yassir Noor amesema sio vyema kwa viongozi ndani ya muungano huo kufarakana ilhali wote wana lengo moja la kunyakua urais wa taifa hili.
Akizungumza katika kampeni zake za kisiasa, Yassir amehoji kwamba Viongozi wa muungano huo wamekita kambi mashinani ili wahakikishe muungano wa Azimio unaunda Serikali baada ya uchaguzi.
Wakati uo huo, mwanasiasa huyo amepuuzilia mbali wapinzani wao akisema hawana lolote la msingi la kuwaambia wakenya mashinani.