Picha Kwa Hisani – Etana Strong One Instagram Page
Msanii wa muziki wa Reggae na Dancehall kutoka Jamaica Etana amefichua kwamba amewashirikisha wanamuziki Wyre na Naiboi kutoka hapa nchini katika albamu yake mpya anayotarajia kuiacha hivi karibuni.
Etana ambaye pia aliteuliwa katika mashindano ya ‘Grammy awards’ amesema hayo kupitia mtandao wake wa Twitter.
Mwanamuziki huyo alitaja jina la album yake na kusema kuwa inaitwa ‘Pamoja’
Etana ambaye alitamba sana kwa wimbo wake “Weakness In me” aliongeza kuwa ameimba kwa lugha ya Kiswahili na kwamba amewashirikisha wasanii wengi maarufu.