Picha kwa hisani –
Wizara ya elimu nchini imesema itatathmini upya mipangilio iliowekwa ya kuwezesha shule za humu nchini kufunguliwa kipindi hiki ambapo kuna mlipuko wa corona.
Akizungumza katika taasisi ya maendeleo ya mtaala nchini KICD Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema wadau wa elimu nchini wamepewa fursa kutoa mapendekezo yao kuhusu suala la kufunguliwa kwa shule za humu nchini.
Magoha amesema wadau wa elimu wana hadi siku ya jumamosi juma hili kuwasilisha mapendekezo hayo , ambayo yatajadiliwa kabla wizara hio kutoa muelekeo mwishoni mwa mwezi huu kuhusu kufunguliwa kwa shule.
Magoha amesema suala la kufanikisha kukaa umbali wa mita moja na zaidi kwa wananfunzi katika shule za humu nchini usambazaji wa barakoa kwa wanfunzi ni changamoto kuu inayokumba wizara ya elimu nchini.