Picha kwa hisani –
Wizara ya Elimu nchini imeungwa mkono katika juhudi zake za kuhakikisha usalama wa Walimu na Wanafunzi unaboreshwa kabla ya shule kufunmguliwa kote nchini.
Mshirikishi wa Chama cha Walimu nchini KNUT kaunti ya Mombasa Dan Aloo amesema ni sharti kipengele cha afya kipewe kipau mbele kabla ya hatua za kuzifungua upya shughuli za kimasomo kuidhinishwa.
Aloo ameshikilia kuwa bila ya fedha kusambazwa shuleni na Walimu waliyoajiriwa na bodi za shule za umma kulipwa, hakuna shughuli zozote za masomo zitakazoendelezwa shuleni.
Hata hivyo ameshikilia kuwa ni sharti swala la usalama na afya ya Wanafunzi na Walimu kutiliwa mkazo kabla ya shule kufunguliwa.
Mapema juma lililopita, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alidokeza kuwa iwapo maambukizi ya virusi vya Corona yatapungua, basi huenda, Serikali ikatangaza kufunguliwa kwa shule.