Picha kwa hisani –
Wizara ya elimu nchini imesema huenda shule za humu nchini zisifunguliwe mwezi januari mwaka ujao kama ilivyotangazwa hapo awali.
Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema kufunguliwa kwa shule kutategemea na hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini akisema iwapo maambukizi yataongezeka zaidi tarehe ya kufunguliwa shule itasongezwa mbele.
Magoha amesema ukosefu wa fedha za kuidhinisha mpango wa kuboresha miundo msingi ya shule za msingi na upili za umma nchini ni changamoto na huenda mazingira ya sasa yakachangia maambukizi miongoni mwa waalimu na wanafunzi.
Magoha amesema kuna haja ya fedha zaidi kutengwa kusimamia mpango huo wa kuboresha mazingira ya shule za umma za humu nchini.