Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ameagiza wizara ya elimu nchini kutoa kalenda ya masomo ya mwaka ujao wa 2021 katika kipindi cha siku 14 itakayotumiwa na wanafunzi wote wa humu nchini watakaporejelea masomo mwakani.
Akitoa hotuba yake katika bunge la Kitaifa Kenyatta amesema wizara ya elimu,ya uchukuzi ,nyumba na maendeleo ya miji watatoa muongozo mpya wa ujenzi wa shule za humu nchini kufikia tarehe mosi disemba ili kuwezesha ujenzi wa madarasa zaidi katika shule za humu nchini.
Kenyatta vile vile amesema katika kipindi cha miezi 24 ijayo wizara ya elimu kwa ushirikiano, serikali za kaunti na hazina ya CDF wataidhinisha rasilimali hitajika za kumaliza uhaba wa madarasa unaoshuhudiwa nchini.
Kwenye suala la usalama Kenyatta amesema usalama wa taifa umeimarika kwani vikosi vya usalama vimefanikiwa kugundua na kutibua njama za magaidi,akisema kwa sasa taifa linakabiliwa na mizozo ya kikabila yanayotokana na siasa mbaya.
Kenyatta aidha amesema licha ya taifa kukabiliwa na janga la corona,serikali imefanikisha ajenda nne kuu za kuimarisha maisha ya wakenya ikiwemo kupiga jeki usalama wa chakula na sekta ya usalishaji,kukabili umaskini maneeo ya mjini sawa na kuwainua vijana kiuchumi.
Akigusia maambukizi ya corona Kenyatta amethibitisha kwamba watu 23 wameaga dunia ndani ya saa 24 zilizopita kutokana virusi vya Corona na sasa jumla ya watu 1,203 wameaga dunia humu nchini kutokana na virusi hivyo.
Kenyatta vile vile amesema watu 919 wamethibitishwa kupata mamabukizi ya virusi hivyo na kwamba kufikia sasa kenya ina jumla ya maambukizi ya corona 66,723.
Kenyatta ameyasema haya kwenye kikao cha pamoja cha maseneta na wabunge katika bunge la kitaifa cha kueleza mafanikia na mikakati ya serikali ambapo amewasilisha ripoti mbali mbali katika bunge hilo ikiwemo ya usalama wa taifa.