Picha kwa hisani –
Wizara ya afya nchini imezindua mashini maalum zitakazotumia teknolojia ya kisasa kukabiliana na majanga ya kiafya.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashini hizo tatu jijini Nairobi,waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema mashini hizo zitasaidia sekta ya afya kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi kwa njia ya kidijitali.
Kagwe vile vile amesema mfumo huo utarahisisha kuwatambua wagonjwa wanaozuru vituo vya afya na fedha wanazotozwa katika vituo hivyo hasa wale walioko kwenye mpango wa bima za afya.
Kagwe vile vile amesema hatua hio itakayofanikisha kuwepo na uwazi katika sekta ya afya nchini.