Wazira ya Afya nchini imeweka wazi kwamba watu 26 wamethibitishwa kuaga dunia katika mda wa saa 24 zilizopita kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika taarifa iliotumwa kwa vyombo vya habari, Wizara hiyo imesema maafa yanayoendelea kunakiliwa nchini kutokana na maambukizi ya Corona yanazidi kutia hofu huku ikiwahimiza wakenya kuchukua tahadhari.
Katika taarifa hiyo, asilimia 15.4 ya maambukizi ya Corona yamenakiliwa ambayo ni idadi ya watu 991 baada ya sampuli 6,417 kufanyiwa uchunguzi na kupelekea idadi hiyo kuongezeka hadi watu 147,147.
Hata hivyo watu 370 wamethibitishwa kupona virusi hivyo na kuchangia idadi ya wale waliopona nchini kufikia watu 99,580 huku Wizara hiyo ikiwahimiza wananchi kuendelea kuzingatia masharti ya kujikinga na Corona.