Story by Our Correspondents-
Wizara ya Afya nchini imezindua zoezi la kuwapa dawa za miyoo watoto wa umri wa kati ya miaka 12 hadi 14 katika shule mbalimbali humu nchini.
Akizungumza wakati wa zeozi hilo mjini Mombasa Mkurungezi wa huduma za matibabu na kingi Dkt Andrew Mulwa amesema dawa hizo zitawasaidia wanafunzi kuboresha afya zao.
Dkt Mulwa amesema zoezi hilo linalenga zaidi ya kaunti 14 nchini ikiwemo kaunti ya Lamu, Tana River, Kilifi, Mombasa, Kwale, Taita Taveta, Narok, Nyamira, Kisii, Migori, Busia, Siaya, Kisumu, na Homa Bay.
Dkt Mulwa amesema zoezi hilo linaendelezwa kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu nchini huku akisema zaidi ya watoto milioni 4 wamelengwa katika zoezi hilo.