Story by Our Correspondents –
Wizara ya Afya nchini imepokea dozi elfu 210 za chanjo ya AstraZeneca kutoka taifa la Poland ili kupiga jeki juhudi za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona nchini.
Mwenyekiti wa Jopokazi la kutoa chanjo ya Corona nchini Dkt Willis Akhwale amesema dozi hizo elfu 210 zitasaidia kuwachanja wakenya ili kufikia azmio la serikali la kuwapa chanjo watu milioni 10 ifikapo mwisho wa mwaka huu.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupokea chanjo hiyo, Dkt Willis amesema kufikia sasa Kenya imepokea dozi 5,146,780 za Corona na takriban watu 3,090,932 wamepokea chanjo hiyo na juhudi hizo zinaendelezwa.