Picha Kwa Hisani –
Idara ya usalama Kaunti ya Kwale imewaomba maafisa wa afya ya jamii Kaunti hiyo kuharakisha lile zoezi la kuwapima virusi vya Corona washukiwa wa uhalifu ambao wamezuiliwa rumande .
Afisa mkuu wa polisi katika gatuzi dogo la Matuga Francis Nguli amesema kuwa kuna idadi kubwa ya washukiwa wa uhalifu wanaozuiliwa rumande wakiwa wanasubiri kupimwa virusi vya Corona .
Wakati uo huo afisa huyo wa polisi ameelezea kuwa ni hatari iwapo washukiwa hao wa uhalifu hawatapimwa ili kujulikana hali zao kwani watahatarisha maisha ya wafungwa wengine ambao wapo gerezani .
Aidha Nguli amesisitiza kusema kuwa idara ya Polisi haiwezi kuwapeleka washukiwa hao gerezani pindi wanapohukumiwa iwapo bado hali zao za virusi vya Corona hazijaweza kubainika .