Story by Our Correspondents –
Wizara ya Afya nchini imewahakikishia wakenya kwamba inafanya kila juhudi kuhakikisha inakabiliana na changamoto mbalimbali zinazoshuhudiwa katika Wizara hiyo ili wakenya waendelea kupata huduma bora za afya.
Katibu katika Wizara ya Afya nchini Susan Mochache, amesema mpango wa kuwajenga uwezo wahudumu wa afya ndio nguzo kuu inayoendelezwa na Wizara hiyo nchini ili kufanikisha azmio la serikali wa afya bora kwa wote.
Hata hivyo Wizara hiyo imedokeza kwamba watu 402 wamethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya Corona baada ya sampuli 6,715 kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara na kupelekea idadi hiyo kuongezeka hadi watu 247,358.
Wakati uo huo Wizara hiyo imehoji kwamba wagonjwa wa Corona 259 wamethibitishwa kupona na idadi hiyo kufikia watu 238,707 huku wengine 10 wakiaga dunia.