Story Our by Correspondents –
Waziri wa Afya nchini Mutahi Kagwe imeweka wazi kwamba maeneo ya baa, mikahawa na burudani yatafunga shughuli zake saa tano usiku kulingana na muongozo mpya uliotolewa.
Katika kikao na Wanahabari jijini Nairobi Waziri Kagwe amesema japo maambukizi ya Corona yameonekana kupungua ni lazima wakenya wapokea chanjo sawa na kuzingatia masharti yote ya kujikinga dhidi ya virusi vya Corona ikiwemo kuvaa barakao.
Waziri Kagwe amewahimiza wahudumu wa afya kuhakikisha wanasambaza chanjo kwa wananchi hasa ile Pfizer na Moderna ambayo ni rahisi kuharibika ili kuafikia azmio la serikali la kuwachanja watu milioni 10 kufikia mwezi Disemba mwaka huu.
Akigusia swala la usafari nyakati za usiku katika sekta ya uchukuzi wa umma, Waziri Kagwe amesema mikakati ya swala hilo linaendelea kwa ushirikiano na Wizara ya uchukuzi nchini na muongozo rasmi utatolewa baadaye.