Picha kwa hisani –
Chama cha Wiper kimemteua Agnes Kavindu Muthama kuwa mgombea wake wa kiti cha useneta wa Machakos kwenye uchaguzi mdogo utakaoandaliwa mapema mwezi machi mwaka huu.
Akizungumza baada ya kumkabidhi vyeti vya uteuzi mgombea huyo,Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka amesema ana imani na uongozi wa wanawake akiwasihi wanachama wa wiper kuhakikisha Bi Agnes anaibuka na ushindi.
Kalonzo amewataka wanasiasa wanapanga kugombea nyadhifa mbali mbali nchini kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022, kuchukua tiketi za chama cha WIPER kuwania nyadhfa hizo.
Uchaguzi mdogo wa useneta wa machakos unatarajiwa kuandaliwa tarehe 18 mwezi machi mwaka huu,na kiti hicho kiliachwa wazi baada ya aliyekuwa seneta wa machakos Boniface Kabaka kuaga dunia mwezi disemba mwaka uliyopita.