Picha kwa hisani –
Kinara wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, amesema mikakati ya kuzindua Muungano mpya wa kisiasa inaendelezwa kwa sasa.
Akizungumza katika eneo la Kabuchai kule kaunti ya Bungoma hapo jana Kalonzo alisema muungano huo utajumuisha vyama mbali mbali ikiwemo chama cha Wiper,ANC, KANU na Ford Kenya.
Kalonzo amesema mwelekeo utakaotolewa na Muungano huo,utasaidia kutatua changamoto mbalimbali nchini ikiwemo kutumiwa vibaya kwa mwananchi katika maswala ya kisiasa.
Kwa upande wake Kinara wa ANC Musalia Mudavadi, muungano huo utasaidia taifa kuimarika kiuchumi na kuchangia amani kwa taifa.