Picha kwa hisani –
Siku moja baada ya Rais wa Tanzania, John Magufuli kutaka wizara ya afya kutokukimbilia chanjo ya Corona, Shirika la Afya Duniani WHO imeitaka nchi hiyo kujiandaa na chanjo ya Corona kama mataifa mengine duniani.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao,mkuu wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshdiso Moeti amesema kuwa Tanzania inatakiwa kutumia mwanya wa upatikanaji wa chanjo kwa faida ya wananchi na kanda ya Afrika mashariki kwa ujumla.
WHO inasema kuwa imekua ikitoa mchango na kuwasiliana na serikali ya Tanzania kuanzia mwanzo wa janga hili la Corona.
Shirika hilo pia limesisitiza Tanzania kutoa takwimu za mwenendo wa Corona nchini Tanzania ili iwe rahisi katika kupambana na kuzuia maambukizi mapya.