
Kinara wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula Ameitaka serikali kuondoa kikosi cha KDF kinachopigana na kundi la kIgaidi la Al- shabab nchini somalia.
Akiongea mjini mombasa Wetangula Amesema kuwa kutokana na kwamba kikosi hicho kanazidisha uvamizi katika ngome kuu za kundi hilo visa vya uvamizi humu nchini vinaonekana kuongeszeka na kupelekea wakenya wengi wasiokuwa na hatia kupoteza maisha yao .
Hata hivyo Amesema kuwa Ni wakati sasa vikosi vya kiusalama nchini kuja na mbinu mpya za kukabila makundi ya kigaidi yanayoendeleza uvamizi Mara kwa Mara hususani sehemu za mipakani.
Kinara huyo aidha ameitaka idara ya usalama nchini kutozembea kwenye majukumu yake na badala yake kuzidisha Ulinzi ziadi ilikuona kwamba taifa hili halididimii kiuchumi.
Taarifa na Hussein Mdune.