Picha Kwa Hisani
Majibizano kati ya mjasiriamali Zarina Hassan maarufu kama Zari na muigizaji wa filamu za Bongo Wema Sepetu bado yanaendelea kwenye mitandao ya kijamii.
Wawili hao ambao wamewahi kuwa katika mahusiano na nyota wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, kwa nyakati tofauti ni paka na chui. Hii inawapa tofauti kati yao na Hamisa Mobetto na Tanasha Donna ambao licha ya wote kuzaa na msanii huyo kwa sasa ni marafiki hadi wanashoneana nguo.
Siku chache zilizopita, Zari na Wema walianzisha upya bifu kwa kujibizana huko mtandaoni, chanzo kikubwa ikiwa ni ile ishu ya kupotea kwa mbwa wa Wema anayeitwa Vanilla Manunu.
Aliyeanza uchokozi ni Zari na ni baada ya shabiki mmoja mtandaoni kumuuliza Zari kama amemuona mbwa wa Wema huko Sauzi ambapo majibu yake yalikuwa, “mbwa amefichwa ndani ila wanafanya kiki tu.”
Picha Kwa Hisani – Wema akiwa na mbwa wake ‘Manunu’
Baada ya kauli hiyo kutoka kwake Zari, Wema akaibuka na andiko lake lililosomoka hivi. “Ok mimi sio kama yeye, I dont need kiki to survive, nguvu anazotumia yeye mimi situmii.”
Wiki iliyopita akiwa katika uzinduzi wa tamthilia ya ‘We Men’, waandishi wa habari walimchokonoa tena Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kwa kumuuliza alijisikiaje Zari alivyoandika kuhusu suala la Manunu (mbwa wake) kuwa ilikuwa ni kiki.
Wema alisema kuwa, “Unajua ukiwa mwizi unahisi kila mtu mwizi, ukiwa muongo unahisi kila mtu muongo na ukiwa mtu mhuni utahisi kila mtu mhuni, so pigia mstari.”
Mashabiki wachonganishi hawakuyakaushia majibu hayo ya Wema na kumpasia tena Zari ambapo shabiki anayejulikana kwa jina la Therealcathe_tz huko Instagrm alimuuliza mama huyo, “Zari wee mbwa wako hajapotea kama wa Wema, halafu Wema alikujibu vibaya Boss Lady.”
Majibu ya Zari yaliyofuata yalikuwa hivi: “… natoa msaada. She could use some free food, naona kabakisha kichwa tu. Hiyo ni njaa, let her eat some food she will be fine.”
Wema sasa katika mtandao wake wa Instagram akaweka video akionyesha vyakula mbalimbali na kuandika, “kugombana na watu wazima ni kujitafutia laana… Na mimi nina heshima sana kwa wakubwa zangu… pia ni mskivu…nafanyia kazi ushauri.”
Unazungumziaje kauli za wanadada hawa?