Picha kwa hisani –
Meneja wa mwananuziki na anayeongoza recording lebo ya WCB, Diamond,
Sallam SK, amefichua mipango ya lebo hiyo kumsaini msanii wao mpya.
Kupitia mkutano aliofanya na wanahabari leo nchini Tanzania, Sallam SK
ameweka wazi kuwa hivi karibuni wanatarajia kumsaini msanii wao mpya baada
ya Zuchu kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.
Kufikia sasa WCB ina jumla ya wanamuziki sita ambao ni Diamond Platnumz,
Rayvanny , Queen Darling , Mbosso Lavalava na Zuchu.