Story by Mwahoka Mtsumi –
Huenda bajeti ya serikali ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni siku ya Alhamsi na Waziri wa Fedha nchini Ukur Yatan ikakosa kusomwa iwapo shinikizo la wabunge la mgao wa CDF litakosa kuafikiwa na serikali.
Hii ni baada ya mvutano kushuhudiwa katika bunge la kitaifa kuhusu hoja ya kusomwa kwa bajeti hiyo baada ya wabunge kudai kwamba watavuruga kikao cha kusomwa kwa bajeti hiyo iwapo serikali haitatoa mgao wa fedha za CDF mapema.
Akichangia hoja hiyo bungeni, Mbunge wa Aldai Cornelly Serem amesema Waziri Yatan amekosa kutimiza ahadi iliyoitowa kwa wabunge kuhusu mgao huo wa CDF, akisema hadi kufikia sasa maeneo bungeni nchini hayajapokea chochote.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya bajeti katika bunge la kitaifa Kanini Kaga tayari amewasilisha ripoti ya kamati hiyo kuhusu makadirio ya bajeti ili wabunge waijadili na kuipitia kabla ya Waziri Yatan kuisoma bajeti ya serikali.
Bajeti hiyo ya mwaka wa kifedha wa 2021/2022 inakisiwa kuwa bajati ya trilioni 2.9 na itasomwa siku ya Alhamis juma hili.