Picha kwa hisani –
Waziri wa Michezo, utamaduni na turathi za kitaifa Bi Amina Mohammed amesema Serikali itafanya kila juhudi ili kulinda makavazi ya kitaifa yaliyoko kaunti ya Lamu.
Amina aliyezuru kaunti ya Lamu, amesema kaunti hiyo hasa visiwa katika vya Manda, Faza na Amu vimekuwa na asilia ya turathi za kitaifa na kutambulika na umoja wa mataifa.
Akizungumza Kisiwani Amu, Amina amasema kuwepo na huduma za bodaboda Kisiwani Amu kumeanza kuathiri historia ya kisiwa cha Amu kinachotambulika kwa huduma ya uchukuzi wa punda.
Amesema ni sharti kila juhudi ziidhinishwe ili kulinda hadhi ya utalii na vile vile kuhakikisha utamaduni wa jamii ya Lamu hauharibiwi huku akiwasihi wazee wa kaunti hiyo kushirikiana na Wizara yake ili kuhakikisha turathi, tamaduni na historia ya wakaazi wa Lamu zinalindwa.