Waziri wa Elimu katika serikali ya kaunti ya Kwale Mangale Chiforomodo amewataka wazazi katika kaunti hiyo kuchukuwa jukumu la kuwalinda watoto wao dhidi ya dhulma za kingono.
Chiforomodo amesema serikali ilizifunga shule ili watoto wa durusu vitabu vyao pamoja na kujikinga na virusi vya Corona na wala sio watoto kuachiwa uhuru wa kurandaranda ovyo.
Wakati ou huo amewaomba wazazi kutowachia uhuru watoto wao kurandaranda mitaani na badala yake kuhakikisha wana watengea muda wa kujisomea majumbani mwao.