Picha kwa hisani
Bunge la Somalia siku ya Jumamosi lilipiga kura kwa kauli moja ya kutokuwa na imani na Waziri mkuu mpya wa taifa hilo Hassan Ali Khaire, na kumtimua mamlakani.
Spika wa Bunge hilo Mohamed Sheikh Abdirahman amesema wabunge waliopiga kura 170 dhidi ya 8 na kumtimua mamlakani Khaire kutokana na kushindwa kuwajibikia majukumu yake hasa ya usalama wa taifa hilo.
Kwa upande wake Rais wa taifa hilo, Mohamed Abdullahi Mohamed amekiri amekubaliana na uamuzi huo uliochukuliwa na bunge la kitaifa ya Somalia licha ya juhudi zake za kulishinikiza bunge hilo kumpa nafasi Khaire.
Rais Abdullahi amesema sasa atalazimika kumteua Waziri mkuu wwengine ili kutekeleza majukumu ya kitaifa kwani nafasi hiyo haiwezi kubaki wazi kwa mda mrefu.