Picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa Wakenya kuunga mkono polisi na mashirika mengine ya usalama ili kudumisha sheria na utangamano, akisema maafisa wa polisi wanatekeleza kazi kubwa kudumisha usalama wa taifa.
Akizungumza eneo la Ngong kaunti ya Kajiado hapo jana Kenyatta amesema serikali imejitolea kuhakikisha huduma ya polisi ya Kitaifa imepewa rasilimali za kutosha ili kutekeleza majukumu yake vyema.
Kenyatta amesema serikali imetilia mkazo taratibu za kushirikisha mashirika mbalimbali katika usimamizi wa usalama kwa kuondoa vizuizi vitakavyotatiza utoaji huduma za usalama siku za usoni.
Kwa upande wake waziri wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i, ambaye pia alizungumza kwenye sherehe hiyo amempongeza Rais Kenyatta kwa kuidhinisha marekebisho ambayo yameimarisha utendaji kazi wa sekta ya usalama nchini.
Gavana wa Benki Kuu ya kenya Dkt Patrick Njoroge na Inspekta Jenerali wa Poilisi Hilary Mutyambai pia walizungumza kwenye sherehe hiyo ya kuzindua ujenzi wa Chuo cha Uongozi wa Huduma ya Polisi ya Kitaifa ujenzi utakaogharimu shilingi bilioni moja.