Picha kwa hisani –
Wizara ya usalama nchini imeahidi kuweka mikakati mwafaka ya kukabiliana na makundi ya kigaidi na uhalifu katika kaunti ya Kwale na Kilifi.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kufanya kikao cha faraga na Gavana wa Kwale Salim Mvurya, Waziri wa usalama nchini Dkt Fred Matiangi amesema tayari serikali imeanzisha mchakato wa ujenzi wa vituo vya huduma kwa vijana kuwajenga uwezo.
Matiangi amesema vituo hivyo vitajengwa katika kaunti ya Kwale na Kilifi ili kuwapa vijana ujuzi utakaowasaidia kujiendeleza kimaisha badala ya kujiingiza katika makundi ya kihalifu.
Kwa upande wake Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema katika kikao hicho cha faragha wamekubali kushirikiana baina ya serikali ya ugatuzi na ile ya kitaifa ili kuimarisha usalama hadi mashinani.