Story by our Correspondent –
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang’i amewahakikishia wakenya kwamba uchaguzi mkuu ujao utakuwa wa amani kwani idara ya usalama imejipanga vyema kuhakikisha wakenya wanashiriki uchaguzi huo bila changamoto.
Matiang’i aliyekuwa akizungumza katika kikao cha kiusalama kilichowaleta pamoja wadau mbalimbali ikiwemo baraza kuu la makanisa nchini NCCK, maafisa wa afya na viongozi wa usalama, amesema uchaguzi huo utakuwa wa utulivu.
Waziri Matiang’i amesema uchaguzi mkuu ujao hautakuwa wa umwagikaji damu bali utakuwa wa amani na usalama huku akiwahikiza vijana kuwa mstari wa mbele katika kuhubiria amani.
Wakati uo huo, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi wakati wa uchaguzi huo na kuwachangia viongozi wanaowapenda kwani usalama utaimairishwa katika kila pembe ya taifa hili.