Story by Mimuh Mohamed-
Jumla ya wanafunzi 38, 797 waliofanya mtihani wa kitaifa wa KCPE wa mwaka 2021 wamechaguliwa kujiunga na shule za upili za kitaifa kufikia tarehe 3 mwezi Mei.
Akizungumza katika makao makuu ya taasisi ya maendeleo ya mtaala KICD jijini Nairobi Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema wanafunzi wengine 214,960 watajiunga na shule za ngazi ya wilaya huku wanafunzi 258,456 wakichaguliwa kujiunga na shule za ngazi ya kaunti.
Magoha aidha amesema wanafunzi 726,311 wanatajiunga na shule za ngazi ya maeneo bunge huku wanafunzi 2,045 wakichaguliwa kujiunga na shule za watu wenye mahitaji maalum.
Kulingana na Magoha wanafunzi 800 kutoka mitaa ya vitongoji duni ni kati ya waliochaguliwa kujiunga na shule za kitaifa na shule za ngazi za wilaya mtawalia.
Waziri Magoha amesema uteuzi huo umezingatia usawa na uwazi na kwamba watahiniwa wote milioni 1.2 waliofanya mtihani huo wamepata nafasi katika shule za upili.