Picha kwa Hisani –
Waziri wa Elimu nchini Profesa George Magoha amesema serikali itasambaza fedha kwa shule zote za msingi na upili hasa zile za umma, kuanzia hapo kesho siku ya Alhamis ili kuhakikisha shuhuli za masomo zinaendelea vyema.
Waziri Magoha amesema wanafunzi wote wa shule za umma hasa wale wa gredi ya 4, darasa la nane na kidato cha nne ambao watarudi shuleni siku ya Jumatatu hasa wale wanaotoka katika familia zisizojiweza watapewa barakoa za bure.
Magoha ameyasema hayo baada ya kufanya mkutano na wadau wa sekta ya elimu katika kaunti ya Kisumu, ambapo amewataka wazazi kuhakikisha wanawanunulia watoto wao barakoa huku akisema taratibu zote za masomo zimepangwa vyema.
Hata hivyo amedokeza kuwa iwapo shuhuli za masomo kwa wanafunzi hao zitaendelea bila ya pingamizi zozote basi mikakati ya kurejea shuhuli zote za masomoni kwa wanafunzi wote nchini itatangazwa.